Jumla ya watu 621, wakiwemo watoto 83, wamekamatwa nchini Chad tangu kuanza kwa maandamano ya upinzani yaliyokandamizwa kwa nguvu na kusababisha vifo vya watu 50, Oktoba 20, 2022 jijini N’Djamena nchini humo.

Waziri wa Sheria, Mahamat Ahmat Alhabo amesema, “Kati ya watu hao 628 waliohojiwa, walipatikana watoto wadogo 83, ikiwa ni pamoja na mtu mmoja, mtoto chini ya umri wa miaka 12 na sheria katika nchi yetu inasema kwamba mtoto chini ya umri wa miaka 12 hahusiki na chochote.”

Waandamanaji nchini Chad. Picha ya The Indian Express.

Mwendesha mashtaka wa N’Djamena, Moussa Wade Djibrine amesema hadi kufikia Novemba 11, 2022, takriban watu 401 wamefikishwa katika mahakama na wengine 220 bado wanasubiri kujibu mashitaka yanayowakabili mbele ya Hakimu aliyepangiwa kusikiliza kesi hizo za za jinai na mambo mbalimbali.

Hata hivyo, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa mamlaka kukiri hadharani kukamata idadi ya zaidi ya watu 600, ambao waliotajwa na NGOs kadhaa za ndani na za kimataifa baada ya maandamano hayo ya kupinga kuongezwa kwa miaka miwili madarakani kwa Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno.

Sokwe wapigwa risasi, watalii waingia hofu
Rais Samia afafanua tozo Daraja la Kigamboni