Migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, imewazuia watalii kuendelea na ziara zao kufuatia mapigano ambayo pia yamewatisha, kuwaua na kuwalemaza sokwe wa milimani, ambao kivutio muhimu zaidi cha Mbuga ya Kitaifa ya Virunga.

Katika siku ya Kimataifa ya Gorilla, kikundi cha wahifadhi wa eneo hilo kilipeleka ujumbe wake kwa vijana wanaoishi karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Virunga huku mapigano kati ya M23 na vikosi vya serikali yakiwanyima walinzi kupata makazi muhimu ya sokwe hao, na kuwaacha bila ulinzi.

Mkuu wa Mabalozi wa Gorilla, Alain Mukiranya amesema, “Lakini pia mbali na hili chaguo lilifanyika ili kuwapata walinzi watoto kwa sababu wao ndio wasimamizi wa baadaye wa urithi huu tunaouhifadhi, wao ndio watakaonufaika na mifumo hii ya ikolojia tunayoilinda.”

Wawindaji wakiwa wamembeba Sokwe. Picha ya REUTERS

Naye mwanafunzi wa Taasisi ya Kalangala Kibumba, Munyampamira Guylain amesema ili kuwalinda sokwe hao, ni lazima kuongeza ufahamu kwa wasaidizi huku akiwaomba na kuwapiga marufuku watu kuwinda sokwe na wanyama wengine na kukata miti katika Hifadhi.

Siku ya Kimataifa ya Sokwe, huadhimishwa kila Septemba 24 na Sokwe wa milimani walio katika hatari ya kutoweka Kongo wanaendelea kutishiwa na ujangili, ukataji miti, na vita.

Wanaaongea lugha tofauti wakutana kusimulia hadithi zao
Watoto 83 wakamatwa wakiandamana