Jeshi la Polisi Mkoani Geita limemfikisha katika Mahakama ya Mwanzo ya Nyankumbu wilayani Geita mtuhumiwa Alfred Joseph (25) kwa tuhuma za kumwibia mwajiri wake Shilingi Milioni 8.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Nyankumbu, Ally Mgomba amesema mtuhumiwa alifanya tukio hilo Machi 28, 2025 kinyume na kifungu 258 na 265 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 (iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022).
Amesema, “baada ya mshtakiwa kuiba fedha kiasi tajwa alitoroka na kwenda kujificha Mkoani Shinyanga, uchunguzi ulipofanyika na kumkamata mtuhumiwa alikiri kuiba na kuzitumia pesa hizo kumlipia mahari mke wake (jina linahifadhiwa) kiasi cha milioni 2, kununua pikipiki MC.236 DXP milioni 2, kununua samani mbalimbali za ndani na kulipia chumba cha kuishi,” amesema.