Ukaguzi wa Ufanisi wa Mamlaka ya Nishati Vijijini – REA, umemulikwa na CAG kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka 2019/2020 ambao umefanyika kwa maombi ya wafadhili, Shirika la Kimataifa la Maendeleo Sweden (Sida).

Machi 2016, Tanzania na Sida waliingia mkataba wa ufadhili wa kutandaza umeme vijijini. Fedha zilitoka SEK 600 milioni (Sh133 bilioni), ambapo uzembe wa kuchelewa kupakua malighafi Bandari ya Dar, ulisababisha REA watumie Sh775.76 milioni kulipa tozo ya uchelewaji (demurrage charge). Fedha za ufadhili zikatumika ndivyo sivyo kwa uzembe.

CAG amebaini kuwa transfoma zilizofungwa uwezo wake ni 50KV, wakati bajeti ilikuwa 100KV ambapo Fedha za wafadhili zilipigwa cha juu na upembuzi yakinifu haukufanyika, udongo haukupimwa, Nguzo kuwekwa pasi na vipimo na Pesa ya upembuzi yakinifu (feasibility study), kupigwa.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG, Charles Kichere.

Ripoti hiyo pia imebaini Wateja 51,425 tu kati ya 98,689 walioomba kuunganishiwa umeme, ndio wameunganishiwa ikiwa ni sawa na asilimia 52.1 ambapo CAG ameandika “nyaraka za SIDA zinaonesha REA walitakiwa kusambaza umeme kwenye nyumba 86,000, hivyo kuhudumia watu 430,000 kupitia gridi ndogo (Green Min and Micro Grid), na wameishia nyumba 17,302, yaani asilimia 20.

Uzembe wa kutohuisha taarifa za utafiti wa mradi, ulisababisha REA kuingia gharama za ziada Sh160 milioni ambapo kuna jumla ya Shilingi 5.94 bilioni, ambazo REA wamekuwa wakizitenga kama bajeti ya matangazo na elimu lakini hakuna maelezo ya zilivyotumika.

Mwaka 2018/2019, REA walitengeneza bajeti ya kununua transfoma na kuunganishia wateja umeme Sh254.8 bilioni. CAG akagundua, gharama halisi ilikuwa Sh117 bilioni, kwa hiyo kulikuwa na udanganyifu wa Sh137.8 bilioni (Ufisadi).

Lingine, REA wilitumia Shilingi 125.57 milioni, kununua transfoma 12 zilizo chini ya kiwango na siasa zikaingia, Tozo ya umeme kwa mwezi ikapitishwa Shilingi 11,000, Serikali ikasema tozo Shilingi 1,000 na kufanya gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko mapato, Umeme ukazima vijijini.

Sehemu kubwa, CAG ameeleza tatizo la uchelewaji, kwani Miradi ambayo ilipaswa kukamilika mwaka 2019/2020, mpaka sasa bado haijakamilika huku hayo yote yakitokea wakati Waziri wa Nishati akiwa Kalemani, ambaye alimpokea Simbachawene kutoka kwa Muhongo Rais akiwa Magufuli.

Watu 30 wauawa katika shambulio kambi ya wakimbizi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo April 10, 2023