Chama cha African National Congress (ANC), kimemchagua tena Rais wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuwa kiongozi wa cha hicho, uliofanyika Johanesburg, Afrika Kusini.

Ramaphosa amekwepa changamoto ya uongozi wa chama chake, siku chache baada ya vuguvugu lililozuka kutaka kumuondoa madarakani kufuatia kashfa ambapo alishutumiwa kuwa alificha pesa katika shamba lake kashfa iliyopewa jina la Farmgate.

Wakati matokeo yanatangazwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Khalema Motlanthe watu waliokuwepo kwenye chumba cha mkutano walipiga kelele za kushangilia .

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Lakini mara alipotaka kuanza kampeni ya muhula wake wa pili, alipata wito wa kutakiwa kujiuzulu baada ya jopo la ushauri kugundua ushahidi wa awali kuwa anaweza kuwa amefanya makosa.

Ramaphosa alikuwa mpatanishi mwandamizi wa ANC wakati wa mazungumzo yaliyopelekea kumalizika kwa amani kipindi cha ubaguzi wa rangi mwaka 1994, ambapo ilimwezesha Nelson Mandela kuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini.

Wakati matokeo yanatangazwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Khalema Motlanthe watu waliokuwepo kwenye chumba cha mkutano walipiga kelele za kushangilia .

Wakandarasi wasiofanya vizuri kukosa miradi
Rais Samia: Lazima tulipe mikopo