Mkataba wa Reli ya kisasa ya SGR awamu ya pili wenye wenye thamani ya dola za kimarekani bil. 2.21 ambao utatekelezwa kwa miezi 48, unatarajiwa kukamiliki ifikapo Decemba 2026.

Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa reli ya kisasa ya SGR awamu ya pili, kipande cha sita (Tabora – Kigoma), ambapo ameongeza kuwa, hali hiyo itafanya jumla ya uwekezaji wa ujenzi wa reli ya SGR kufikia kiasi cha dola za kimarekani bil. 10.04.

Amesema, ”Hizi Trilioni 23.3 za kitanzania au bilioni 10.04 zote ni mikopo kwa hiyo wale wanaosema awamu hii imekopa sana ndiyo awamu ambayo imejenga reli yote pia, na tusingeweza kujenga kwa fedha za ndani ilibidi tukope tujenge.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ameongeza kuwa, ”lakini ukiacha reli kuna mambo kadhaa ambayo yamefanywa ndani ya awamu hii na tusingeweza kufanya lazima tukope na tunakopa ili tujenge leo kwa maendeleo endelevu ya leo na baadae kwahiyo kila pale tunapohisi panafaida tutaendelea kukopa.”

”Waseme wamu hii imekopa sana na wasema pia ndiyo awamu iliyojenga sana wasijifanye kama wanaume wa kiislamu Quran imewaambia kuoa wanne ruhusa lakini hawamalizi ayah ruhusa lakini inafatiwa na nini?”sasa na hawa wanasema awamu hii imekopa sana lakini imefanya nini hawafiki huko,” amebainisha Rais.

Aidha Dkt. Samia amezidi kusema, ”Kwa mfano mwezi huu kulikuwa na vimaneno sijui hakuna pesa serikalini pesa kwasababu mikopo tulikopa imechelewa ya kufanyia kazi hizi lakini mbili kuna mikopo iliyo ‘mature’ kwa pamoja miwili na imebidi yote tulipe lakini kuna certificate za miradi mikubwa ambayo imekuja imebidi tulipe kwahiyo kwa kuweka heshima za nchi yetu lazima tulipe mikopo.”

ANC kuongozwa tena na Ramaphosa
Brighton and Holve Albion: Mac Allister hauzwi