Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Arusha Jumatatu Julai 26 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema mkoa huo umebeba jukumu la kuandaa mazishi ya Mghwira, ambapo amesema mama Anna Mghwira atapumzishwa kwenye makazi yake ya milele Julai 26 mwaka huu jijini Arusha.
Mghwira alifariki dunia jana Julai 22 katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.