Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kilichotokea leo katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha Anna Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa, hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa Taifa.

Amewaomba Wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina. 

Shangazi mjumbe mpya bodi ya wakurugenzi Simba SC
Rais Samia Akutana Na Tony Blair Ikulu Dar