Uongozi wa Klabu ya Arsenal umesimamisha mazungumzo ya mkataba na Meneja wa kikosi cha klabu hiyo Mikel Arteta ili kuepusha usumbufu kipindi hiki ambacho timu ipo bize katika mbio za kuusaka ubingwa wa England.

Arteta amebakiza zaidi ya miaka miwili katika mkataba wake wenye thamani ya Pauni 8.3 milioni kwa mwaka, ambao alisaini kabla ya mwisho wa msimu uliopita.

Akizungumza kuhusu mustakabli wake Arsenal, Arteta alisema kwa sasa sio muda muafaka wa kuzungumza kuhusu masula ya mikataba, kwasababu itamtoa mchezoni.

“Kwa sasa ninachotaka ni kushinda kila mechi ili tufikie malengo yetu ambayo tunakata msimu huu,” alisema Arteta.

Endapo Arsenal itabeba ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 19, thamani ya Arteta itapanda maradufu.

Baadhi ya Klabu kama Manchester City, FC Barcelona na PSG zinatajwa kumfuatilia Meneja huyo kutokana na kazi kubwa anayoendelea kuifanya akiwa na Arsenal msimu huu 2022/23.

Kwa mujibu wa ripoti, PSG iko katika mchakato wa kuachana na Meneja wao wa sasa Christophe Galtier baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Arsenal haina shaka kuhusu mkataba wa Arteta kwa sababu wanaamini Mhispania huyo atasaini tu baada ya kupewa sifa na uongozi.

Saba wakamatwa na nyara meno ya tembo, nyama pori
Kocha Simba SC ashikilia hatma ya Dilunga