Kocha Mkuu mpya wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa atatumia nguvu kubwa kuwashawishi wachezaji wake watumie uwezo wote walionao kupata matokeo.
Arteta ambaye aliwahi kucheza ndani ya Arsenal na alikuwa nahodha amesema kuwa anaamini wachezaji wanaweza kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mashabiki na timu kiujumla.
“Nitawashawishi wachezaji kucheza kwa nguvu na kutumia uwezo wao wote walionao kupata matokeo chanya,Hatua kwa hatua ninaamini kwamba tutafikia malengo yetu na mafanikio tutayaona yatakayo tutambulisha sisi katika wakati ambao tunauhitaji,” amesema Arteta
Kabla ya kutua Arsenal, Arteta alikuwa ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi Manchester City akifanya kazi na Kocha Mkuu, Pep Guardiola.
Arteta amechukua mikoba ya Unai Emery ambaye alipigwa chini hivi karibuni baada ya kudumu kwa muda wa miezi 18 amepewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu kukinoa kikosi hicho.
Pia kocha huyo ambaye aliwahi kucheza ndani ya Arsenal na alikuwa nahodha amesema kuwa anaamini wachezaji wanaweza kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mashabiki na timu kiujumla.