Shirikisho la soka nchini TFF limesema katika kukuza maendeleo ya soka la Tanzania, FIFA wapo kwenye mpango wa kujenga vituo vya michezo hapa nchini.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ameyasema hayo leo kwenye mkutano mkuu wa TFF unaofanyika jijini Dar es salaam, ambao umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpira.

Rais huyo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amesema kuwa FIFA wameahidi kujenga uwanja mmoja hapa nchini.

“FIFA wameahidi kujenga uwanja mmoja hapa nchini na tumekubaliana kujenga vituo viwili vya Soka (Technical Centres) kwa maeneo ya Tanga na Kigamboni-Dar es Salaam, ujenzi ambao mchakato wake umeshaanza na mapema mwakani ujenzi utaanza,” amesema Karia.

Simba yaanza kazi kimyakimya
Wataalam wa mipango waagizwa mawazo ya ubunifu