Meneja wa Klabu ya Arsenal Mikel Arteta amepongeza kitendo cha Meneja wa zamani wa Klabu hiyo Arsene Wenger kuwa sehemu ya walioshuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumatatu (Desemba 26).

Arsenel ilicheza nyumbani Uwanja wa Emirates jijini Lindon dhidi ya West Ham Utd iliyokubali kichapo cha 3-1.

Arteta amesema uwepo wa Arsene Wenger ulikuwa motisha kwa kila mmoja klabuni hapo hasa wachezaji wake vijana, ambao walionesha kupanbana na kupata ushindi huo nyumbani.

Amesema Mzee huyo ameifanyia mengi mazuri Arsenal na asilimia kubwa ya wachezaji wa sasa walikuwa wakimshuhudia ama kumsikia, lakini uwepo wake Uwanjani kama shuhuda wa mchezo dhidi ya West Ham Utd uliongeza kitu kwenye ushindi wao wa jana.

“Uwepo wake hapa umeleta kitu kikubwa sana kwa wachezaji wetu vijana, ninaamini walipambana kwa ajili ya Klabu, pia walihitaji kumuonesha sehemu ya matunda yake ambayo kwa sasa yamekomaa,”

“Hata mimi nilifurahishwa na uwepo wake hapa, naamini Uongozi ulifanya kusudi kubwa la kumleta aje kushuhudia mchezo wetu, ambao kwa hakika ulikuwa mgumu sana, lakini tumeshinda.” amesema Arteta.

Wenger, aliondoka Arsenal kama Meneja mwaka 2018, akiingoza Klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20, huku akitwaa ubingwa wa Ligi ya England mara tatu (1997–98, 2001–02 na 2003–04).

Ubingwa wa Kombe la FA mara Saba: 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, 2013–14, 2014–15 na 2016–17

Ngao ya Jamii mara Saba: 1998, 1999, 2002, 2004, 2014, 2015 na 2017

Mabao ya Arsenal katika mchezo dhidi ya West Ham Utd, yalifungwa na Bukayo Saka, Gabrel Martineli na Eden Nketiah huku bao la kufutia machozi la West Ham Utd Saïd Benrahma.

Ushindi huo unaendelea kuiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England Arsenal, kwa kufikisha alama 40 baada ya kucheza michezo 15.

Mwinyi alia na changamoto mahitaji ya chakula
Watano wafariki kwa ajali Iyovi