Meneja wa washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London ‘Arsenal’ Mikel Arteta amesema hatobadili malengo ya kufanya usajili wakati wa dirisha dogo (Mwezi Januari 2021), licha ya kupata ushindi mara mbili mfululizo.
Arsenal waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Brighton and Hove Albion lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Alexander Lacazette kipindi cha pili, ikiwa ni suhindi wa pili mfululizo ukitanguliwa na ule dhidi ya Chelsea mwishoni mwa juma lililopita.
Arteta alifunguka kuhusu kutobadili mpango wake wa kufanya usajili mara baada ya mchezo huo wa uganini kwa kusema: “Hapana, matokeo ya michezo hii miwili hayabadili mipango yetu kuelekea dirisha la usajili.” alijibu Arteta alipoulizwa kama matokeo hayo yana maana yoyote kuelekea dirisha la usajili la mwezi Januari 2021.
Isco kuhamia England, Wijnaldum kutimkia La Liga
Arsenal hawakupata ushindi katika michezo saba wakiwa katika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi ya England, wakati wa Christmas lakini kutoka hapo wamefanikiwa kumfunga Chelsea na Brighton and Hove Albion na kufanikiwa kuchupa hadi kwenye nafasi ya 13 kwenye msimamo huo.