Halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga kiasi cha Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya Jiji ifikapo tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu.

Ujenzi wa mahakama hiyo ni kwa lengo la kushughulikia kesi mbalimbali za wafanyabiashara wataokaidi kulipa kodi za Serikali au ushuru wa vibanda vya biashara zao kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji hilo Dkt. Maulid Madeni ambapo amesema kuwa kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutasaidia kuongeza mapato katika Halmashauri kwa kuwa tayari zipo sheria ndogo ndogo zitakazo saidia kupitisha hukumu kwa watakao patikana na hatia ya kuikoseshea mapato Halmashauri.

“Katika Mahakama itakayoanzishwa tutaweza kutoa hukumu kwa masaa machache ikiwa ni faini ama kifungo kwa wataopatikana na hatia ya kuinyima mapato halmashauri” amesema Dkt. Madeni.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro ameunga mkono juhudi za Serikali ya awamu tano katika ukusanyaji wa mapato na ameahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Mkurugenzi katika operesheni yake ya ukusanyaji wa mapato.

Breaking News: Waitara atetea Ubunge wake, atangazwa kuwa mshindi Ukonga
Video: CCM yaibuka na ushindi asilimia 95 Monduli