Klabu ya Associazione Sportiva Roma (AS Roma) imetangaza kuchangia kiasi cha pesa kwa ajili ya kusaidia kundi la wakimbizi ambalo limeendelea kuingia katika nchi za barani Ulaya kutoka mataifa mbali mbali duniani.

Raisi wa klabu ya AS Roma, Jim Pallotta ametangaza mpango huo, kwa kuamini mchezo wa soka unahitajika kuonyesha dhamira ya kusaidiana na serikali za nchi kadhaa za barani Ulaya ambazo zimeafiki kuwahifadhi wakimbizi hao.

Pallotta amesema klabu yake itachangia kiasi cha Euro 575,000 ambazo ni sawa na paund 418,000.

Amesema yeye pamoja na viongozi wenzake wanaendelea kuumizwa na janga la wakimbizi hao, ambao wameonekana kuhitaji msaada kutokana na nchi zao kuingia kwenye matatizo ya vurugu za kisiasa pamoja na vita vya wenywe kwa wenywe.

Hata hivyo AS Roma inakua klabu ya pili kutangaza kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaoingia kwa wingi barani Ulaya, baada ya FC Bayern Munich ya nchini Ujerumani kuweka hadharani mpango wa kuchangia paund 730,000.

Nayo kamati ya kimataifa wa Olympic IOC, imetangaza kutoa paund million 1.3 kusaidia janga hilo.

Wakimbizi wanaoingia kwa wingi katika mataifa ya barani Ulaya wanatoka kati nchi za Afrika pamoja na mashariki ya kati.

Clyne Asisitiza Utulivu Kabla Ya Safari Ya Old Trafford
Chadema Yaruka Viunzi Tuhuma Za Udini Dhidi Ya Lowassa