Maaskofu watatu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) wametengwa na kanisa hilo kwa tuhuma za usaliti zinazohusishwa na mambo ya kisiasa.
Maaskofu waliotajwa kutengwa na kanisa hilo ni, Askofu wa Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, DKT Alex Malasusa, Dk Solomon Masangwa wa Dayosisi ya kaskazini ya kati na Dkt Lucas Mbedule wa wa Dayosisi ya kusini Mashariki.
Ambapo katika mkutano wa Baraza la Maaskofu wa KKKT, uliofanyika Aprili 24 na 25 jijini Arusha umejadili masuala mbalimbali ikiwemo kufanya tathmini ya waraka wake wa sikukuu ya Pasaka uliotolewa Machi 24 mwaka huu.
Uongozi wa Baraza hilo la maaskofu wa KKKT umewataka maaskofu hao watatu waliotengwa na kanisa kuandika barua yenye maelezo ya kukubali au kukataa kuwa walishiriki kuandaa waraka huo uliohusishwa na mambo ya kisiasa yenye uchochezi dhidi ya viongozi kwa wananchi wake na ikiwa hawatafanya hivyo hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.
Pia maaskofu hao hawataruhusiwa kushiriki shughuli zozote za kiroho ndani na nje ya Dayosisi hizo mpaka pale suala lao litakapojadiliwa upya.
Aidha mchakato huo ni kufuatia waraka uliotelewa mwaka huu ukizungumzia mambo mbalimbali ya kisiasa na kuonesha nchi haipo katika muelekeo mzuri ambapo waraka huo ulipangwa usisomwe mpaka pale utakapopitiwa upya na shirika zote nchini kupunguza baadhi ya mambo ambayo yalionekana hayakukaa sawa.
Baadhi ya Viongozi walikiuka agizo hilo na kusoma waraka huo hali ambayo ilileta mzozo na mtazamo tofauti kwa taifa na kupitia usaliti huo umeongeza mzigo kwa Kanisa katika kuiombea nchi amani na viongozi wao.