Shirika la Ndege Nchini – ATCL, linatarajia kupata ndege mpya moja aina ya Boeing B737-9MAX na ndege ndogo aina ya Dash 8 Q300, mwishoni mwa mwezi Septemba, 2023 ambapo matengenezo yake yanatarajiwa kuwa yamekamilika na kurejea katika ratiba zake za kawaida za utoaji wa huduma.
Akizungumza hii leo Septemba 4, 2023 Bungeni Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema uwepo wa Ndege hizo kutaiwezesha ATCL kuanzisha safari zake katika kituo cha Pemba kwa tija na ufanisi wa Taifa.
Amesema, “niwahakikishie Serikali inafahamu na inatambua uzito uliopo wa umuhimu wa kupeleka ndege hizo pemba na ndiomaana zimeshaanza mchakato na sisi tunaongeza kasi zaidi ili muweze kusafiri kama ambavyo inatakiwa.”
Hata hivyo, Kihenzile ameongezea kuwa baada ya Kukamilika kwa usadifu wa uwanja wa Ndege Mkoa wa Singida, hatua inayofuata ni kujua mahitaji muhimu ili kuweza kuufanyia kazi uwanja huo.