Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia ndugu Kenedy John (35) mkazi wa Dar es salaam kwa tuhuma za kuwawekea Dawa za kulevya wanawake kisha kuwabaka, kuwaingilia kinyume na maumbile pamoja na kuwaibia mali zao.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Jonathan Shanna ambaye amesema kuwa mhalifu huyo amekili kufanya uhalifu huo kwa kipindi cha muda mrefu katika mkoa wa Mwanza, Arusha, Geita Dar es salaam na Mara.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa daktaria amethibitisha kuwa mwanaume huyo amekuwa akiwawekea madawa ambayo hutumika kuwapa wagonjwa wa kichaa ili kuwatuliza.

Ameongezea kuwa amekuwa akiwahadaa wadada kwa kuwanunulia vinywaji mbalimbali kisha kudondoshea vidonge hivyo vya kulevya na kuwabaka pamoja na kuwafanya kinyume na maumbile na kuwaibia mali zao.

Kamanda Jonathan ameomba vyombo vya habari kumuanika mhalifu huyo ambaye hivi karibuni atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayomkabili kwani amekuwa akifanya vitendo zaidi ya mnyama.

Mbali na mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake chenye weledi, uadilifu na uwezo mkubwa, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akiwemo wanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sonia Fanuel kwa kosa la kujihusisha na wizi wa kutumia funguo bandia (Master Key).

 

Mgambo washusha kichapo kwa vijana wakitaka wajiunge nao
Madam Rita aanika wanachowafanyia washiriki wa BSS nyuma ya pazia