Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli amechaguliwa tena kwa mara ya nne nne kuwa Naibu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Duniani (ITUC).

Atwoli amechaguliwa kwa wadhifa huo katika Kongamano la 5 la mashirika ya vyama vya wafanyakazi linaloendelea mjini Melbourne, Australia.

Mwanaharakati huyo wa kuwatetea haki za wafanyakazi alichaguliwa bila kupingwa na wajumbe 2000 katika kinyang’anyiro kikali, na kupewa muhula wa miaka minne ITUC, ambayo ina makao yake makuu mjini Brussels, Ubelgiji.

“Nafasi mliyonipa sio rahisi. Unanituma kupigania wanaume na wanawake wanaofanya kazi popote pale walipo duniani. Sitawaangusha kamwe Nitasimamia maslahi yenyu na kutoa maisha yangu kwa ajili yenyu kila mara,” amesema Atwoli


Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli akiwahutubia wajumbe wa ITUC Australia. Picha: ITUC.

Awali, Atwoli alichaguliwa bila kupingwa katika Kamati ya Sifa ya Wanachama Saba, ndani ya usanifu wa ITUC, ambayo huamua ni nani anahitimu kuwa mjumbe wa shirikisho. Kamati hiyo pia ina majukumu ya ripoti kuhusu muundo wa wajumbe mbalimbali kwa kila nchi pamoja na kiwango cha uwezo wao wa kupiga kura.

Kando na kuchaguliwa kuwa Naibu Rais, Atwoli pia alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la ITUC ambapo atakuwa akiwakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kupendekezwa na mjumbe kutoka Tanzania na kuungwa mkono na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Mauritius miongoni mwa mataifa mengine ya Afrika.

Kaduguda: Simba SC ipo tayari kwa Uchaguzi
Jezi ya Ubelgiji yapigwa marufuku QATAR