Umoja wa Afrika(AU), umelaani mabadiliko ya serikali kinyume na katiba nchini Burkina Faso, baada ya maafisa wa ngazi za chini kumpindua Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba ambaye naye Januari 24, 2022 alimpindua Rais mteule, Roch Marc Christian Kabore.

Nchi hiyo, sasa itakuwa chini ya Kapteni Ibrahim Traore (34), ambaye amevunja Serikali, kusimamisha na kuweka katiba ya mpito huku akisema wamemuondoa Damiba baada ya kushindwa kukabiliana na uasi unaozidi kuota mizizi kinyume na ahadi zake za kuifanya nchi kuwa salama.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa Burkina Faso wamepongeza hatua hiyo, ambapo mmoja wao Francois Kaboré, amesema, “Damiba hakuweza tena kusimamia suala la usalama, watu wengi walikufa na wahalifu walikaribia miji mikubwa kwa hiyo, watu hawakufurahishwa na hilo.”

Wanajeshi waasi wa Burkina Faso, wakilinda lango la kituo cha Televisheni cha Taifa huko Ouagadougou. (Picha na AP/Sophie Garcia)

Raia mwingine, Alidou Pitroipa yeye anasema mapinduzi si njia ya kutatua kutoelewana na viongozi wa kisiasa na kuongeza kuwa, “Kama kuna tatizo kati ya askari, jadilianeni baina yenu, kutafuta suluhu na sio kupindua madaraka maana yake, kwa hali ya aina hii, hatujui itakapoisha.”

Mkuu wa Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat alisema ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuzuka upya kwa watu waliofukuzwa kinyume na katiba nchini Burkina Faso, na kwamba kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba ifikapo Julai 2024 kutafanya nchi hiyo kuwa na utulivu.

Mtawala wa zamani wa kikoloni wa Burkina Faso Taifa la Ufaransa, aliwaambia raia wake huko Ouagadougou, wanaoaminika kuwa kati ya 4,000 na 5,000, kusalia nyumbani, wakati wakitafuta namna ya kuwashughulikia huku Umoja wa Ulaya ukionyesha kusikitishwa na matukio hayo.

Nyerere day: Mashujaa wa Afrika na mafanikio ya AU
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Octobar 2, 2022