Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Ahmed Msangi amesema ajali ya basi la Super Shemi (T 874 CWE) linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mbeya lililogongana na Hiace (T 368 CWQ) uso kwa uso leo Septemba 21, 2016 imesababishwa na uzembe wa madereva kwa kushindwa kuzingatia sheria za barabarani.

Akizungumza na Dar24 amesema ajali hiyo imetokea kwenye eneo la Nhungumalwa, Mwamaya Makutano wakati dereva wa Hiace alipoingia kwenye barabara kubwa bila kuangalia hivyo kuligonga basi kubwa na kusababisha vifo vya watu 10 waliofariki eneo la tukio huku wengine 3 wamefariki baada ya kufikishwa hospitali na kufanya jumla ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa 13 na majeruhi 11.

 

 

 

Sakata la viwanja Kibaha, Waziri Mkuu atoa onyo
FIH Yaahidi Kufufua Mpira Wa Magongo Nchini