Kesi inayo wakabili viongozi wa klabu ya Simba Evans Aveva na Geofrey Nyange kaburu, imetajwa tena hii Leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam.
Jopo la mawakili wa upande wa jamuhuri likiongozwa na Leonard Swai limesema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Aveva na Kaburu walifikishwa mahakamani hapo Julai 3 mwaka huu na kusomewa mashtaka 5 yakiwemo ya kujilipa madeni ya kiasi cha dola 300,000 na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu, na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande.