Mashabiki wa soka kisiwani Unguja wameushutumu uongozi wa chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA), kufuatia matumizi ya tiketi za kuingilia uwanjani kupita muda wake.

ZFA walitumia tiketi zilizokwisha muda wake katika michezo ya ufunguzi ya ligi kuu ya soka visiwani huo kanda ya Unguja iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Amaan.

Mashabiki hao wa soka walishangazwa kununua tiketi za mchezo  kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya KMKM na badala yake wakauziwa tiketi zilizoandikwa mchezo wa Jang’ombe boys na Taifa ya Jang’ombe, mchezo ambao tayari umeshachezwa tangu tarehe 30/07/2017.

Mbali na hilo tiketi wameuziwa shilingi elfu mbili wakati bei iliyoandikwa kwenye tiketi hizo ni shilingi elfu moja

Mashabiki hao wamesema ni aibu kwa chama cha soka ngazi ya taifa kushindwa kujiandaa kikamilifu, hususan suala la uchapishaji wa tiketi zinazokwenda muda, hivyo wameutaka uongozi wa ZFA kujireekebisha.

Kundi la P-Square bado hali si shwari, Paul aibua mapya
Aveva, Kaburu waendelea kusota rumande