Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maji, utakaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha.

Mkutano huo utafanyika kuanzia Desemba 13 – 14 , 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha ukiwashirikisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu, Naibu Waziri wa Maji, MarryPrisca Mahundi na wadau mbalimbali.

Dhumuni la mkutano huo ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso kutaka kuwashukuru wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji kwa jitihada wanazozifanya za kuwezesha upatikanaji wa hitaji hilo na kuwapongeza kwa mchango wao mkubwa katika kuwezesha mafanikio yaliyopatikana Nchini.

Aidha, wadau hao pia watapewa fursa ya kujadili, kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la Mwaka 2023 na Mpango Mkakati wa Wizara.

Benchikha amuachia msala Seleman Matola
Casemiro aongeza mzuka Manchester United