Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Bodi ya Wakala wa UsambazajiMaji Vijijini (RUWASA) pamoja na Menejimenti yake kuanisha miradiyote ya maji vijijini yenye changamoto na kujua gharama zake na namnaya kutatua changamoto hizo.
Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya RUWASA pamoja na Menejimenti katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma, Awesu Amewataka ifikapo mwezi Machi 2021 miradi yote yenye chagamoto iwe imefanyiwa kazi na kukamilikakwa kutoa huduma kwa wananchi yenye uhakika.
“Hakikisheni mnafanya kazi kwa kushirikiana kama timu moja ya Wizara ya Maji ili tuweze kutekelezalengo letu la kuwahudumia watanzania na kuwapatia majisafi, salama na yenye kutosheleza,”amesema Aweso.
Aidha, amewataka RUWASA kuongeza na waimarishe ushirikiano na Chuo cha Maji kwa kuwatumiawataalam wanaotoka katika chuo hicho katika usimamizi wa miradi ya maji wanayoitekeleza.
Katika hatua nyingine , Aweso ameutaka uongozi wa RUWASA kuainisha miradi yote iliyokamilika kwa kutumiawataalam wa ndani (Force Account) na kuhakikisha miradi yote ya maji nchini inakuwa endelevu kwakuunda vyombo vya watumia maji vyenye uwezo wa kusimamia na kuendesha miradi hiyo.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Prof. Idrissa Mshoro ameishukuru serikali kwa kuiwezesha RUWASA kwa namna mbalimbali katika kutekeleza majukumu yake na kumhakikishia Mh. WaziriAweso kuwa RUWASA itahakikisha inatekeleza majukumu yake ipasavyo.
Pia, amesema Bodi imeielekeza RUWASA kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account) ili miradi ikamilike kwa wakati na wananchi waweze kupatahuduma hiyo mapema zaidi.