Uongozi wa Azam FC umetoa taarifa kuhusu kuzuia kwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi kutumika kwa ajili ya michuano ya kimataifa iliyo chini ya Shirkisho la soka Barani Afrika ‘CAF’.
‘CAF’ wameizuia Namungo FC kutumia uwanja huo kwa sababu za kukosa vigezo vya kutumika kwenye michuano ya kimataifa upande wa vilabu, lakini wawakilishi hao wa Tanzania walikua wakiutumia kwenye michezo ya awali ya Kombe la Shirikisho.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC, Zakaria Thabith, amesema bado hawajapokea barua yoyote kutoka ‘CAF’ kuhusu Uwanja wao wa Azam Complex kuzuiliwa kuacha kutumika katika michuano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika hatua za makundi kutokana na kutokidhi vigezo.
Zakaria amesema taarifa za watu kusema sababu za kukatazwa Uwanja wao kutumika ni kutokana na Uwanja huo kuwa mdogo, hizo sababu siyo za kweli.
“Vipimo vya kawaida vya CAF na FIFA inatakiwa Uwanja mkubwa uwe na Vipimo vya (Mita 120 urefu, Mita 90 Kona Hadi Kona) na kiwanja kidogo kiwe na Vipimo (Mita 90 urefu, Mita 45 Kona Hadi Kona) wakati kiwanja Cha Azam Complex vipimo vyake ni (Mita 105 urefu, na Mita 68 Kona Hadi Kona) ikifanana vipimo na Uwanja wa Mkapa.”
Zakaria amesema wanaendelea kufuatialia swala Hilo ili kufahamu sababu zilizopelekea Klabu ya Namungo FC kuzuiliwa na ‘CAF’ kutokuutumia Uwanja huo wa Azam Complex katika michezo ya hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.
Namungo FC kesho walikua wautumie Uwanja wa Azam Complex Chamazi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramid kutoka Misri, hivyo mchezo huo umehamishiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.