Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe, amesema kuwa wataonyesha ukubwa wa timu hiyo kwa vitendo uwanjani kwa kupata matokeo mazuri.

Timu hiyo inaendelea na kambi huko Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 na ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal Julai 14 ikapata ushindi wa mabao 3-0.

Kazi ya mipango ya, Youssouph Dabo raia wa Senegal ambaye ni Kocha Mkuu wa Azam FC na msaidizi Bruno Ferry.

Ibwe amesema kuwa kila msimu kunakuwa na utofauti jambo ambalo wanalichukulia kwa ukubwa kutokana na uimara walionao.

“Kila msimu kunakuwa na hali ya utofauti nasi hilo tunatambua kwa sababu ni timu kubwa basi tutaonyesha ukubwa wetu kwa vitendo uwanjani.

“Maandalizi yanayofanyika ni kwa ajili ya mechi zote za msimu ujao kitaifa na kimataifa na kwenye upande wa wachezaji wote ni bora na wapo tayari kupambania nembo ya Azam FC,” amesema Ibwe.

EWURA kuwachukulia hatua wanaoficha mafuta
Ally Kamwe: Kuna kazi nzito 2023/24