Benchi la Ufundi la Azam FC limetoboa siri ya ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata dhidi ya Kagera Sugar jana Jumatano, kwenye uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera.
Azam FC ilichez akwa tahadhari kubwa huku ikiwaheshimu wenyeji wao Kagera Sugar, na kufanikiwa kuchomoza na ushindi huo kupitia mabao ya mshambuliaji Prince Dube aliyefikisha bao lake la nane ndani ya Ligi Kuu ilikuwa ni dakika ya 27 huku Braison Raphael yeye alifungua akaunti ya mabao ya Azam FC dakika ya 20.
Mwamuzi wa kati aliwapa mkwaju wa penalti Kagera Sugar dakika ya 42 ilijazwa kimiani na Peter Mwalyanzi huku maamuzi ya utata dakika ya 86 kwa mpira uliopigwa na Martin Kapama wa Kagera Sugar kufika kwenye mwili wa Abdul Haji,’Hamahama’ kutafsri kwamba ni faulo.
Akizungumza kwa niaba ya benchi la ufundi la klabu hiyo yenye maskani yake makuu Chamazi jijini Dar es salaam, Kocha msaidizi Vivier Bahati amesema haikuwa rahisi kuibuka na ushindi kwenye uwanja wa ugenini hasa unapoocheza na kikosi cha Kagera Sugar.
Kocha Vivier amesema:”Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana kuweza kupata matokeo ila mwisho wa siku wamefanikiwa.
“Akili zetu kwa sasa ni kwenye mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kazi bado inaendelea.”
Kwa ushindi huo Azam FC imefikisha alama 40, zinazoendelea kuwaweka kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kucheza michezo 22 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 12 na alama zake ni 24.
Azam FC itacheza dhidi ya Mwadui FC ambayo inapambana kujinasua kushuka daraja, Uwanja wa Mwadui Complex mwishoni mwa juma hili.
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Mwadui FC ipo nafasi ya 18, ikiwa imekusanya alama 15.