Azam FC inaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kocha mkuu wa timu, Stewart Hall amepiga ‘stop’ kikosi chake kucheza mechi za kirafiki na sasa ni ufundi tu hadi msimu utakapoanza.

Stewart amesema, mechi 18 ambazo ni za kirafiki pamoja na za mashindano zimetosha kabisa kujua kipimo cha wachezaji wake.

“Kwa sasa ni ufundi tu, narekebisha mambo mengine madogo madogo, hatutacheza tena mechi za kirafiki, nahitaji kuwa na kikosi changu kwanza kwa maandalizi zaidi,”alisema Stewart.

Katika mechi za kirafiki ambazo Azam FC wamecheza, wamepoteza mechi moja tu waliyofungwa na JKT Ruvu mabao 2-1 na nyingine walishinda pamoja na kutoa sare.

Barakah Da Prince Apewa Shavu Na Rapa Mkubwa Kenya
Clyne Asisitiza Utulivu Kabla Ya Safari Ya Old Trafford