Klabu ya Azam FC imeiilipa klabu ya Union Sportive Goree pesa ya usajili wa mshambuliaji Alassane Diao ambaye alitangazwa kujiunga nao mwanzoni mwa mwezi Julai.
Baada ya Diao ‘B52’ kutangazwa kujiunga na Azam FC Kama mchezaji huru, klabu ya US Goriee ya Senegal ilitishia kuishitaki Azam FC FIFA kwa kuchukua mchezaji wao bila kumlipia ada ya uhamisho wakati ana mkataba.
“Tumewalipa dola kadhaa ili kuepusha mgogoro usio wa lazima. Unajua Ligi ya Senegal imesogezwa mbele hivyo kuchelewa kuisha ila kimsingi mkataba wa Diao unatamka kwamba unaisha 2023, lakini wao wamepata faida ya ligi kusogezwa wakadai bado ana mkataba vinginevyo mkataba wake ungeisha tangu mwezi Juni” alisema kiongozi mmoja wa juu wa Azam.
Union Sportive Goree ni klabu ya michezo inayomilikiwa na Mwnasiasa maarufu ambaye alikuwa Meya wa Goree mwaka 2002 Augustin Senghor.
Senghor ndiye Rais wa klabu lakini pia Rais wa Shirikisho la Mpira la Senegal, pia Senghor ni makamu wa Rais wa kwanza wa Shirikisho la Mpira la Afrika CAF kati ya wale makamu wa tatu wa Rais wa CAF. US Goree inamiliki pia timu ya mpira wa kikapu (Basketball).