Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa hakuna timu ambayo haitapenda kuwa na mchezaji kama Makabi Lilepo ambaye anahusishwa kujiunga na timu hiyo.
Nyota huyo anatajwa kuwa katika rada za Azam FC inayopambana kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24.
Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa, wanatambua ubora wa Lilepo pamoja na uwezo kutajwa kutawakiwa na Azam FC.
“Timu kubwa inasajili wachezaji wakubwa na unaona kwa sasa wanahusishwa wachezaji wengi ikiwa ni pamoja na Lilepo hilo kwetu hakuna tatizo wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
“Kwa namna timu yetu ilivyo usajili wake utakuwa ni mzuri wenye manufaa kwa timu, uwepo wa Feisal Salum ukiongezea na nyota wengine wazuri utafanya kila mechi tuonyeshe ushindani mkubwa na kupata matokeo mazuri,” amesema Ibwe.
Azam FC imegotea nafasi tatu katika msimamo wa Ligi Kuu msimu wa 2022/23, ikiwa na alama 59 baada ya kucheza michezo 30.