Kuelekea mchezo wa 33 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mabingwa Simba SC, Klabu ya Azam FC itawakosa wachezaji wake, Salum Abubakar *Sure Boy*,  Prince Dube na nahodha Agrey Morris kutokana na sababu mbalimbali.

Taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha George Lwandamina zinaeleza kuwa Sure Boy na Agrey Morris wanasumbuliwa na Malaria wakati Prince Dube akiwa bado hajapona vizuri jeraha lake.

Kwa upande wa Simba itawakosa wachezaji wake Bernard  Morrison ambaye ameenda nchini kwao Ghana kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia, Jonas Mkude ambaye suala lake bado halijamalizika, Miraji Athumani ambaye amepata majeruha mazoezini na Ibrahim Ajibu anayesumbuliwa na Malaria.

Tayari Simba SC imeshatwaa Ubingwa wa Tanzania Bara tangu Jumapili (Julai 11), baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0, nakufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote inayoshiriki ligi hiyo msimu huu.

Mchezo wa kesho utakua na umuhimu mkubwa kwa Azam FC inayohitaji kumaliza nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Msimu huu 2020-21.

Juventus yaichomolea Chelsea
Watanzania wapo salama Afrika Kusini