Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linawashikilia watu wawili akiwemo baba mzazi wa mwanafunzi wa miaka 12 aliyetaka kuozeshwa mtoto na wazazi wake.

Kamnada wa Polisi mkoni Arusha Jonathan Shanna amsema wanawashikilia watu wawili akiwemo mwananume aliyetaka kumuoa binti huyo ambaye ana umri wa miaka 45.

Amesema tukio hilo lillilotokea kata ya Musa wilayani Arumeru ambapo kabla hawajafanikiwa mpango wa kumuozesha mwanafunzi huyo, wananchi kwa kushirikiana na Poilisi waliweza kuwakamata.

”Hivi karibuni kuna wimbi limeibuka la watu hususani wenye tamaa ya mahari katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo nyumbani kutokana na Corona, kutumia nafasi hiyo kuozesha wanafunzi” amesema Kamanda Shanna

”Na kama kuna yeyote aliyepokea mahari kwa mtoto wake hakika tutampeleka jela na kama kuna yeyote alikula hela ya ushenga kwa kufanikisha zoezi hilo ovu nasema ataitapika, kama wananchi wa kawaida au jirani ndugu na jamaa alikula chakula katika sherehe hiyo kitamtokea puani” amesisitiza Kamanda Shanni

PSG kuwatema Cavani, Silva
Waziri Jafo amlilia Mkurugenzi wa Babati, Hamisi Malinga