Baba mzazi wa Nahodha na Mshambuliaji wa Kikosi cha Argentina Lionel Messi amekana madai kwamba mwanawe amekubali kuondoka Paris Saint-Germain msimu utakapaomalizika na atatimkia Saudi Arabia msimu ujao.

Taarifa zinadai Messi alikubali kusaini mkataba wenye thamani ya Pauni 522 katika klabu ya Saudi Arabia, Al-Hilal.

Baba wa mchezaji huyo anayefahamika kwa jina la Jorge aliandika ujumbe uzito kupitia mtandao wa kijamii: “Hakuna chochote kwani taarifa hizo za uongo. Uamuzi hautafanyika kabla ya Messi kumalizia msimu akiwa na PSG. Msimu ukiisha tutakaa chini na kujadili na uamuzi utafuata.

Siku zote kuna uvumi na wengi hutumia jina la Messi vibaya, lakini tunawahakikishia hakuna jambo kama hilo. Messi hajasaini mkataba na timu yoyote ya Saudi Arabia.”

Wakati huohuo, PSG imekataa kuzungumzia tetesi za Messi kuhusishwa na Al-Hilal na kusisitiza bado nyota huyo ana mkataba utakaodumu hadi Juni 30.

Iliripotiwa Jumanne iliyopita kwamba mke wa Messi, Antonela Rocuzzo hataki familia yake ihamie Saudia Arabia kwa sababu wanapenda kuishi Ulaya.

Vilevile taarifa zilidai Messi ana mpango wa kubaki Ulaya huku na huenda akarejea Barcelona, lakini ataangalia kwanza hali ya kiuchumu inayoikabili.

Messi anatumikia adhabu ya kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili baada ya kusafiri hadi Saudi Arabia na familia yake bila ya ruhusa ya klabu.

Messi alikwea pipa kwenda huko kutokana na ishu za kibiashara akiwa kama balozi wa nchi hiyo. Hata hivyo PSG ilichukizwa na kitendo chake kukwepa mazoezi ya timu. Tayari nyo ta huyo keshaomba radhi.

Vitambulisho ni suala la usalama wa Taifa - Majaliwa
Serikali mbioni kuanzisha miradi biashara ya Kaboni