Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikilia Baba na watoto wake wakiume wawili kwa tuhuma za kumuua mkewe 57 kwa kushirikiana na watoto hao baada ya polisi kupokea simu kuoka kwa watuhumiwa kuwa kuna mtu amejinyonga.
Aidha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na madaktari lilifanya uchunguzi wa mwili wa marehemu na kugundua kuwa chanzo cha kifo chake sio kujinyonga na ndipo jeshi hilo likawashikilia watuhumiwa hao.
Akizugumza na Dar24Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Sophia Jongo amesema kuwa watuhumiwa hao wamekili kumuua bibi huyo kwa kumkaba na kumvuta ulimi mpaka umauti kumkuta, huku wakieleza sababu ni kuchoka kumuuguza bibi huyo kwa muda mrefu.
Aidha watuhumiwa hao bado wameshikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi na kufikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake juu yao.
Sambamba na hayo Jeshi hilo limejipanga kuzunguka Wilaya zote za mkoani hapo kwa lengo la kutoa elimu ili kuepukana na matukio kama hayo, lakini pia kushirikiana na mapolisi kata kwa kutoaa taarifa za matukio yote ya kiaharifu.
Hata hivyo amewahasa wananchi kuwapenda wazazi na kuachana na imani zpotufu.