Mshambuliaji kutoka DR Congo Heritier Ebenezer Makambo leo Alhamisi {Agosti 05} amefika kwa mara ya kwanza kwenye kambi ya klabu ya Young Africans, Avic Town Kigamboni jijini Dar es salaam.

Makambo amefika kambini hapo baada ya kutambulishwa rasmi na Uongozi wa Young Aftrcans, katika kipindi hiki cha usajili wa msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Makambo aliyerejea klabuni hapo kwa mara ya pili, baada ya kuondoka mwaka 2019, akiwa kambini Avic Town alikutana na kusalimiana na baadhi ya wachezaji wa Young Africans na kupiga nao picha.

Kabla ya kurejea Young Africans, Makambo alivunja mkataba na klabu ya AC Horoya ya Guinea iliyomsajili akitokea kwa Wananchi.

Baba na mtoto wadaiwa kumuua mama
RC Makalla azindua Kampeni ya usajili wa walipakodi