Kampuni ya Bakhresa Food Product ambao ni watengenezaji wa bidhaa za Azam, wamewaomba wateja wake kurejesha juice za Mango zilioonekana kuwa na makosa katika tarehe ya kutengenezwa kwake.

Hivi karibuni, picha ya bidhaa hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na nembo inayoonesha kuwa imetengenezwa Oktoba 19 mwaka huu, tarehe ambayo kiuhalisia bado hatujaifikia.

Kutokana na mkanganyiko huo, Uongozi wa kampuni hiyo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, imewaomba radhi wateja wake na kueleza kuwa makosa hayo ni ya kibinadamu na mashine kwani tarehe sahihi iliyopaswa kuonekana ni 19/09/2016 na sio 19/10/2016.

img-20161013-wa0047

“Tunawaomba wateja wote ambao walinunua bidhaa hizo kurejesha pale walipozinunua kwani tunafanya marejesho ya bidhaa hiyo,” imeeleza taarifa hiyo. “Uongozi unaomba radhi wateja wake na watumiaji wa bidhaa zetu adhimu kwa usumbufu wowote wanaoupata kwa urejeshwaji huu wa bidhaa,” imeongeza.

Uongozi huo umeeleza kuwa umetoa taarifa kwa Mamlaka zote zinazosimamia ubora wa vyakula nchini na kwamba wanawakikishia wananchi wote kuwa bidhaa zao ni bora kwa matumizi ya binadamu.

Dkt. Shein Aipongeza NEC kwa Kutoa Elimu ya Mpiga Kura
Diwani Chadema anaswa na dawa za kulevya, bunduki