Hofu iliyokua imetanda huko Emirates Stadium, ya kuhisi huenda kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere akakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya majuma matatu, imekua kweli.

Wilshere alikadiriwa kukaa nje ya uwanja kwa majuma yasiyopungua matatu baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kulia akiwa katika maandalizi ya kucheza mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Chelsea, ambao ulimalizika kwa The Gunners kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Taarifa kutoka kwenye kitengo cha utabibu klabuni hapo zimeainisha kwamba, jeraha la kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, litahitaji umakini hadi kupona kwake, na huenda likachukua muda usiopungua miezi miwili.

Hii haitokua mara ya kwanza kwa Wilshere kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja, kwani aliwahi kukutana na mikasa kama hiyo kuanzia mwaka 2009.

Jeraha ambalo linaonekana kuchukua nafasi kubwa ya kumuweka nje ya uwanja kiungo huyo wa kiingereza, ni maumivu ya kifundo cha mguu ambapo ilijitokeza kwa zaidi ya mara nane huku majeraha mengine yaliyowahi kumsumbua ni nyama za paja, mgongo pamoja na sehemu ya pembani ya paja.

Orodha Ya Majeraha Ambayo Yamewahi Kumkabili Wishere Tangu Mwaka 2009.

October 2009 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Matano)

January 2010 – Nyama Za Paja (Nje Majuma Matano)

November 2010 – Mgongo (Nje Majuma Mawili)

August 2011 – Kifundo Cha Mguu (Nje Miezi 14)

February 2013 – Pembezoni Mwa Paja *Hip* (Juma Moja)

March 2013 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Manne)

May 2013 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Saba)

October 2013 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Mawili)

January 2014 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Mawili)

March 2014 – Kifundo Cha Mguu (Nje Miezi Miwili)

October 2014 – Kifundo Cha Mguu (Nje Majuma Mawili)

November 2014 – Kifundo Cha Mguu (Nje Miezi Mitano)

August 2015 – Kifundo Cha Mguu (Makadirio Ya Miezi Miwili)

29 Waitwa Kuunda Stars Itakayocheza Dhidi Ya Nigeria
Pardew Amkana Coloccini