Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha amemuonya Mshambuliaji wa timu hiyo, Jean Baleke kushindwa kutumia nafasi za mara kwa mara ambazo anazipata kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kauli hiyo ameitoa kuelekea katika mchezo dhidi ya Wydad Casablanca unotarajiwa kufanyika Jumamosi (Desemba 09) nchini Morocco, ambapo kocha huyo amesema michezo kama hiyo inahitaji nafasi moja na kufunga kwani hazitokei mara kwa mara.

Hata hivyo kauli hiyo inamlenga nyota wa Simba SC Jean Baleke ambaye katika mchezo uliopita dhidi ya Jwaneng Galaxy ugenini nchini Botswana alishindwa kuzitumia vyema nafasi ambazo alizipata ambazo zilikuwa zaidi ya tatu na kama angetumia hata moja basi angeipa ushindi timu yake.

Simba SC katika Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi wameshindwa kupata ushindi katika mchezo wowote kati ya michezo miwili waliyocheza ambapo yote waliambulia sare.

Benchikha amesema kuwa: “Michezo ya Ligi ya Mabingwa inahitaji Mshambuliaji kutumia nafasi kila inapopatikana kutokana na aina ya michezo inavyokuwaga huwa nafasi hazipatikani mara kwa mara.

“Tunakwenda kucheza ugenini dhidi ya Wydad ni timu kubwa ambayo ni ngumu kukubali kufanya makosa sasa kwa Mshambuliaji unapopata nafasi ya kufunga lazima itumiwe vyema hii sio michezo ya ligi ni michezo ya Ligi ya Mabingwa lazima waelewe hilo,” amesema Benchikha

Vijana wajadili njia za kuondoa umasikini, utegemezi
Majeruhi wa mafuriko watibiwa bila kupewa rufaa