Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amewataka Vijana wanaoibukia katika nafasi za uongozi nchini, kujadili namna ambavyo Taifa na bara la Afrika linawezaje kuondokana na umasikini na utegemezi wa kiuchumi.

Prof. Mkumbo alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku sita ya vijana viongozi zaidi ya 60 kutoka nchini Tanzania na nchi ya Afrika kusini, katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Amesema, ni wajibu vijana kujifunza namna ambayo itasaidia Bara la Afrika na nchi yetu kwa ujumla kuondokana katika wimbi la umaskini na kujitegemea na kuingia katika nchi zenye ustawi mzuri wa uchumi.

Prof. Mkumbo ameongeza kuwa, uongozi wa Karne ya 21 umejikita katika ukombozi wa kiuchumi jambo litakalo saidia wananchi kutapa kipato Kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa Kwa ujumla na kwamba viongozi vijana wanapaswa kutafuta mbinu za kuondoka katika umaskin na utegemezi.

“Katika uongozi wa Karne ya 21 , huko tulipitoka tulikazania suala la ukombozi wa kisiasa lakini mkazo mkubwa katika ulimwengu wa Leo lazima tuweke mkazo katika suala la ukombozi wa kiuchumi maana tunahitaji watu wetu wapate kipato na kazi,” alisema.

Awali, Mkuu wa Shule ya uongozi ya Mwl. Julius Nyerere, Prof. Mercelina Chijoriga, alisema mafunzo hayo yanatolewa Kwa vijana waopo katika sekta zilizo rasmi na zisizo rasimi ambapo watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo kuleta mapinduzi chanya katika uchumi wa Bara la Afrika.

Kwa upande wake mnufaika wa mafunzo hayo, Bernad Gatty ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo na mbinu mbadala la kupambana na umaskini kupitia raslimali zilizopo nchini na Bara la Afrika Kwa ujumla.

Wasanii Tz washauriwa kuungana kuwasaidia wahanga Manyara
Baleke achimbwa mkwara Simba SC