Balozi Mbarouk ampokea katibu mkuu Jumuiya ya Madola Zanzibar
3 years ago
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amempokea Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipowasili Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mhe. Scotland yupo nchini kwa ziara maalumu ya kukutana na kumfahamisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan maudhui ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi Juni 2022.