Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani – IPU, Dkt. Tulia Ackson.
Balozi Mbarouk aliambatana na Mabalozi watatu waliohusika kwenye Kampeni ya IPU, walipoenda kumpongeza kwa ushindi huo na kumhakikishia Ushirikiano wa Wizara katika utekelezaji wa Majukumu yake mapya.
Mabaloz haoi watatu ni pamoja na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Seiman Suleiman.
Wengine ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva, Balozi Hoyce Temu pamoja na Balozi Robert Kahendaguza.