Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea Kusini kupitia Shirika lake KOFIH imeendelea kuimarisha Sekta afya hapa nchini kwa kusaidia vifaa Tiba, Mafunzo, pamoja na gari la wagonjwa katika mkoa wa Pwani.

Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Tanzania, Song Geum- Young amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo Ambulance moja na Vifaa Tiba Kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.

Aidha, licha ya Kukabidhi gari hilo la wagonjwa Balozi huyo wa Korea Kusini amekubali ombi la waziri wa TAMISEMI ,Selemani Jafo kuboresha miundombinu ya Hospitali hiyo ya Wilaya.

Shirika la KOFIH linatekeleza mradi huo ndani ya mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miaka sita ambapo mradi huo unatarajiwa kupunguza tatizo la vifo vya mama wajawazito.

Hata hivyo, akipokea Gari hilo la wagonjwa waziri Jafo ameishukuru Serikali ya Korea Kusini kwakuwa rafiki wa Tanzania.

Dkt. Bashiru aikana kauli yake, adai Bashe, Nape sio watukutu
Fabian Schar kuimarisha ukuta Newcastle United