Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Malawi zimetambua umuhimu wa kuimarisha biashara za mipakani ambao pia ni mkakati wa kukuza utalii.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika jijini Mbeya.

Amesema kuwa kongamano hilo litawezesha kuzungumzia fursa na changamoto za kibiashara ikiwemo shughuli za utalii baina ya nchi hizo.

Aidha, kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema kuwa kongamano hilo mbali ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Malawi, pia ni kichocheo cha kukuza utalii kwa mikoa ya mipakani.

Amesema Serikali kwa sasa inaboresha miundombinu ya  maeneo ya vivutio vya utalii vya Nyanda za Juu kusini hivyo Kongamano hilo ni linafanyika muda muafaka kwa vile litawavutia   wafanyabiashara wa utalii wa kuwekeza katika fukwe za ziwa Nyasa

Naye, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi, Henry Musa amesema kuwa imeandikwa historia kubwa kati ya nchi hizo mbili na anaamini kuwa kongamano hilo litasaidia nchi hizo kufunguka kiuchumi.

Dkt. Bashiru asema kuwanyamazisha Nape, Bashe ni kuuwa chama
Video: Bila Nape, Bashe CCM itakufa, TANESCO yazikatia umeme taasisi nyeti