Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watu wote waliovamia Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja.
 
Ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
 
Amesema kuwa taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.
 
“Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia halafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki,”amesema Dkt. Kigwangalla
 
Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
 
  • Lugola amtwisha zigo jingine Inspekta Sirro
 
  • Kangi Lugola azikalia kooni kampuni zilizochota fedha za mradi wa NIDA
 
  • Video: Chadema wajilipua, Polisi waliohusishwa mauaji ya Akwilina huru
 
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine

DC Mofuga asimamia zoezi la kuteketezwa kwa moto nyumba sita
Imran Khan aongoza kura za uchaguzi mkuu