Shabiki wa Yanga ameanguka na kupoteza fahamu baada ya Prisons kuishindilia timu hiyo bao la pili kupitia Mohammed Mkopo, dakika ya 62.

Prisons ilipata bao la pili ikiipiku Yanga ambayo ilitangulia kuliona lengo la timu hiyo, lakini ikasawazisha na kufunga bao la pili, hali iliwachanganya mashabiki wa Klabu hiyo ya Jangwani.
Bao hilo, lilimuangusha shabiki huyo anayeelezwa kusafiiri kuipa nguvu Yanga mkoani Mbeya.
       
Watu wa huduma ya kwanza wakifika haraka na kumpa huduma stahiki.
Mpira ni dakika zote za maamuzi, mwisho Yanga ilisawazisha kwa mkwaju wa penalti kupitia Simon Msuva.
Haijajulikana kama shabiki huyo alifanikiwa kuliona bao hilo la pili la mkwaju wa penati ambalo lingeweza kuwa tiba kwake wakati huo.
Chanzo: salehjembe

FC Barcelona Yamuaibisha Gary Neville Hispania
Azam FC Noma Sana, Yatwaa Ubingwa Zambia