Beki wa kati kutoka nchini Hispania Sergio Ramos anaamini bao lake la kwanza akiwa na Paris Saint-Germain ‘PSG’ huenda likawa bao bora, miongoni mwa mabao aliyowahi kufungwa siku za nyuma.
Beki huyo alifunga bao lake la kwanza tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu, kwenye mchezo wa Ligi ya Ufaransa dhidi ya Reims, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.
Ramos alianza kwa mara ya pili kwenye kikosi cha kwanza cha PSG baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha tangu alipotua klabuni hapo akitokea Real Madrid.
“Nina furaha sana kwa ushindi huu na kwa bao langu la kwanza na timu hii,” alisema Ramos akiiambia Amazon Prime Video.
“Nimefurahi nilicheza kwa dakika 90. Ninapenda kuungwa mkono na mashabiki. Ni vizuri kuchukua alama tatu.”
“Hili ni bao langu la kwanza na PSG na ninatumani kutakuwa na mengi zaidi. Jambo muhimu ni kuimarika kimwili siku baada ya siku.”
Naye Meneja wa Paris Saint-Germain ‘PSG’ Mauricio Pochettino, ambaye timu yake iliendeleza ushindi nyumbani ameonyesha furaha yake kwa Ramos.
“Nina furaha kwa ajili yake. Ni muhimu kwake kumaliza mchezo,” amesema Pochettino.