Waziri wa mambo ya nje wa Austria Alexander Schallenberg amefanyiwa vipimo na kukutwa ana maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo inaonekana alivipata kwenye Mkutano wa Umoja wa Ulaya siku ya Jumatatu
Maambukizi ya Schallenberg yanaaashiria kwamba huenda Baraza la Mambo ya Nje la Jumuiya ya Mataifa ya Ulaya lililofanyika mapema wiki hii lilikuwa kama chanzo katika kueneza Virusi vya Corona.
Waziri wa Mambo ya nje wa Ubelgiji Sophie Wilmes, jana alisema kuwa anajitenga kwa muda kutokana na kujishuku kuwa na dalili za Covid 19.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Austria amesema Schallenberg pia alihudhuria Mkutano wa Baraza la Mawaziri siku ya Jumatano lakini
mawaziri walikuwa wamevaa barakoa.
Baraza la mawaziri la Austria limekuwa na hofu katika kipindi cha chini ya majuma mawili yaliyopita baada ya mtu wa karibu wa Kansela wa Austria Sebastian Kurz kupimwa na kukutwa na maambukizi ya Covid 19.
“Kama hatua ya tahadhari watumishi wote wa serikali watafanyiwa vipimo siku ya Jumamosi” amesema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Austria.