Klabu ya Barcelona imeamua kurudi tena mahakamani kuishitaki PSG pamoja na wawakilishi wa Neymar kuhusu kiasi cha pesa ya ziada ambayo Barcelona waliitoa kwa wawakilishi wa mchezaji huyo wakati akienda PSG baada ya mchakato wa usajili kukamilika.

Barcelona bado hawajaridhika na jinsi mchakato huo ulivyokwenda pamoja na ukweli kwamba tayari Neymar ameanza kuvaa jezi ya PSG.

Klabu hiyo inaamini kuna rushwa ilihusika kwenye upande mmoja wa usajili huku baba mzazi wa Neymar naye akihusishwa katika kesi hiyo ambapo Barcelona wanahitaji kiasi cha euro milioni 8.6 kama fidia.

Baba mzazi wa Neymar na upande wa wawakilishi wa mchezaji huyo wanadaiwa walipokea zaidi ya euro milioni 26 wakati wa mchakato wa usajili huo kitu ambacho kimewafanya Barcelona kuhisi kuna rushwa ilitendeka.

Tayari kesi hii imepelekwa mbele ya mahakama ya FIFA na pande zote tatu yaani Barcelona, baba mzazi wa Neymar na PSG watakutana siku ya Jumanne kuanza kujadili kesi hii.

 

 

 

Watu milioni 17 duniani hupoteza maisha kwa magonjwa ya moyo
Man City kumkosa Aguero kwa wiki nne