Mshambuliaji wa Man City striker Sergio Aguero amepata mpasuko katika mbavu, kufuatia ajali ya gari aliyoipata akiwa mjini Amsterdam nchini Uholanzi alipokwenda kuhudhuria tamasha la muziki.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo kwa ajili ya kuzungumza mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea utakaochezwa mwishoni mwa juma hili, Guardiola alithibitisha taarifa za mchezaji wake kupata ajali ya gari sambamba na majibu ya vipimo.

“Jambo kubwa ambalo tumethibitishiwa kupitia vipimo vyake, ni kuhusu mpasuko uliopo kwenye mbavu zake, na itamchukua siku kadhaa kupatiwa matibabu, lakini sijafahamu itakua ni muda gani ambao atakua nje ya uwanja.”

Akizungumza kupitia kituo cha Radio Metro, Aguero alisema ” Dereva wa teksi aliekua akimuendesha hakuona ukingo wa baranaba, hali ambayo ilisababisha kupatikana kwa ajili iliyompa madhara katika mwili wake.

“Nimevunjikia mbavu. Ninakabiliwa na maumivu makali. Nina imani nitakuwa fit siku kadhaa zijazo.”

Katika hatua nyinginen Guardiola pia akazungumzia maendeleo ya beki wake wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Benjamin Mendy kwa kusema, anaendelea kupatiwa matibabu, na huenda akashindwa kumtumia hadi mwezi Aprili 2018, wakati michezo ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

“Mendy atakua nje ya uwanja hadi kwenye nusu fainali za ligi ya mabingwa barani Ulaya, na Aguero, sijafahamu bado itamchukua muda gani kurejea uwanjani kutokana na mimi binafsi kutokua na utaalamu wa kitabibu”. Alisema Guardiola

Mendy anakabiliwa na jeraha ya goti, na tayari ameshasafirishwa kuelekea mjini Barcelona nchini Hispania kwa matibabu zaidi.

Video: 50 Cent aeleza alivyokataa pesa za Trump
Ligi Kuu TZ Bara: Mechi saba kuchezwa kesho, moja jumapili